| ← Psalms (14/150) → |
| 1. | Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema. |
| 2. | Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. |
| 3. | Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja. |
| 4. | Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti Bwana. |
| 5. | Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki. |
| 6. | Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge, Bali Bwana ndiye aliye kimbilio lake. |
| 7. | Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! Bwana awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi. |
| ← Psalms (14/150) → |