| ← Psalms (137/150) → |
| 1. | Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni. |
| 2. | Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu. |
| 3. | Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. |
| 4. | Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni? |
| 5. | Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau. |
| 6. | Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu. |
| 7. | Ee Bwana, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ya Yerusalemu. Waliosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini! |
| 8. | Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi. |
| 9. | Heri yeye atakayewakamata wadogo wako, Na kuwaseta wao juu ya mwamba. |
| ← Psalms (137/150) → |