Psalms (136/150)  

1. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2. Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3. Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4. Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5. Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7. Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8. Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
9. Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
10. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
11. Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
12. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
13. Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
14. Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
15. Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
16. Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
17. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
18. Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
19. Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
20. Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
21. Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
22. Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
23. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
24. Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
25. Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
26. Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

  Psalms (136/150)