| ← Psalms (134/150) → |
| 1. | Tazama, enyi watumishi wa Bwana, Mhimidini Bwana, nyote pia. Ninyi mnaosimama usiku Katika nyumba ya Bwana. |
| 2. | Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi Bwana. |
| 3. | Bwana akubariki toka Sayuni, Aliyezifanya mbingu na nchi. |
| ← Psalms (134/150) → |