Psalms (133/150)  

1. Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.
2. Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
3. Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele.

  Psalms (133/150)