← Psalms (132/150) → |
1. | Bwana, umkumbukie Daudi Taabu zake zote alizotaabika. |
2. | Ndiye aliyemwapia Bwana, Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo. |
3. | Sitaingia hemani mwa nyumba yangu, Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu; |
4. | Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi, Wala kope zangu kusinzia; |
5. | Hata nitakapompatia Bwana mahali, Na Shujaa wa Yakobo maskani. |
6. | Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata, Katika konde la Yearimu tuliiona. |
7. | Na tuingie katika maskani yake, Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake. |
8. | Ee Bwana, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako. |
9. | Makuhani wako na wavikwe haki, Watauwa wako na washangilie. |
10. | Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako, Usiurudishe nyuma uso wa masihi |
11. | Bwana amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalihalifu, Baadhi ya wazao wa mwili wako Nitawaweka katika kiti chako cha enzi. |
12. | Wanao wakiyashika maagano yangu, Na shuhuda nitakazowafundisha; Watoto wao nao wataketi Katika kiti chako cha enzi milele. |
13. | Kwa kuwa Bwana ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani yake. |
14. | Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele, Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani. |
15. | Hakika nitavibariki vyakula vyake Wahitaji wake nitawashibisha chakula. |
16. | Na makuhani wake nitawavika wokovu, Na watauwa wake watashangilia. |
17. | Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi |
18. | Adui zake nitawavika aibu, Bali juu yake taji yake itasitawi. |
← Psalms (132/150) → |