| ← Psalms (130/150) → |
| 1. | Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia. |
| 2. | Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. |
| 3. | Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? |
| 4. | Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe. |
| 5. | Nimemngoja Bwana, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. |
| 6. | Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi. |
| 7. | Ee Israeli, umtarajie Bwana; Maana kwa Bwana kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi. |
| 8. | Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote. |
| ← Psalms (130/150) → |