| ← Psalms (129/150) → |
| 1. | Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa, |
| 2. | Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza. |
| 3. | Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao. |
| 4. | Bwana ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki. |
| 5. | Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni. |
| 6. | Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea. |
| 7. | Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, Wala mfunga miganda kifua chake. |
| 8. | Wala hawasemi wapitao, Amani ya Bwana ikae nanyi, Twawabariki kwa jina la Bwana. |
| ← Psalms (129/150) → |