| ← Psalms (128/150) → |
| 1. | Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake. |
| 2. | Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema. |
| 3. | Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako. |
| 4. | Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana. |
| 5. | Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; |
| 6. | Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli. |
| ← Psalms (128/150) → |