| ← Psalms (126/150) → | 
| 1. | Bwana alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto. | 
| 2. | Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, Bwana amewatendea mambo makuu. | 
| 3. | Bwana alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi. | 
| 4. | Ee Bwana, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini. | 
| 5. | Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. | 
| 6. | Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake. | 
| ← Psalms (126/150) → |