| ← Psalms (125/150) → |
| 1. | Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. |
| 2. | Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele. |
| 3. | Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu. |
| 4. | Ee Bwana, uwatendee mema walio wema, Nao walio wanyofu wa moyo. |
| 5. | Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, Bwana atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli. |
| ← Psalms (125/150) → |