| ← Psalms (124/150) → |
| 1. | Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa, |
| 2. | Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia. |
| 3. | Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu |
| 4. | Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu; |
| 5. | Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo. |
| 6. | Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. |
| 7. | Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. |
| 8. | Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi. |
| ← Psalms (124/150) → |