| ← Psalms (123/150) → |
| 1. | Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni. |
| 2. | Kama vile macho ya watumishi Kwa mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu. |
| 3. | Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu sisi, Kwa maana tumeshiba dharau. |
| 4. | Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, Na dharau ya wenye kiburi. |
| ← Psalms (123/150) → |