| ← Psalms (122/150) → |
| 1. | Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana. |
| 2. | Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu. |
| 3. | Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana, |
| 4. | Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za Bwana; Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la Bwana. |
| 5. | Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi. |
| 6. | Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao; |
| 7. | Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako. |
| 8. | Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe. |
| 9. | Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu, Nikutafutie mema. |
| ← Psalms (122/150) → |