Psalms (120/150)  

1. Katika shida yangu nalimlilia Bwana Naye akaniitikia.
2. Ee Bwana, uiponye nafsi yangu Na midomo ya uongo na ulimi wa hila.
3. Akupe nini, akuzidishie nini, Ewe ulimi wenye hila?
4. Mishale ya mtu hodari iliyochongoka, Pamoja na makaa ya mretemu.
5. Ole wangu mimi! Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki; Na kufanya maskani yangu Katikati ya hema za Kedari.
6. Nafsi yangu imekaa siku nyingi, Pamoja naye aichukiaye amani.
7. Mimi ni wa amani; Bali ninenapo, wao huelekea vita.

  Psalms (120/150)