| ← Psalms (12/150) → |
| 1. | Bwana, uokoe, maana mcha Mungu amekoma, Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu. |
| 2. | Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki; |
| 3. | Bwana ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Nao ulimi unenao maneno ya kiburi; |
| 4. | Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu? |
| 5. | Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema Bwana, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya. |
| 6. | Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba. |
| 7. | Wewe, Bwana, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele. |
| 8. | Wasio haki hutembea pande zote, Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu. |
| ← Psalms (12/150) → |