| ← Psalms (116/150) → |
| 1. | Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. |
| 2. | Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. |
| 3. | Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni; |
| 4. | Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. |
| 5. | Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. |
| 6. | Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa. |
| 7. | Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako, Kwa kuwa Bwana amekutendea ukarimu. |
| 8. | Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka. |
| 9. | Nitaenenda mbele za Bwana Katika nchi za walio hai. |
| 10. | Naliamini, kwa maana nitasema, Mimi naliteswa sana. |
| 11. | Mimi nalisema kwa haraka yangu, Wanadamu wote ni waongo. |
| 12. | Nimrudishie Bwana nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea? |
| 13. | Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana; |
| 14. | Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote. |
| 15. | Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake. |
| 16. | Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu. |
| 17. | Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la Bwana; |
| 18. | Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote. |
| 19. | Katika nyua za nyumba ya Bwana, Ndani yako, Ee Yerusalemu. |
| ← Psalms (116/150) → |