Psalms (114/150)  

1. Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2. Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake.
3. Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma.
4. Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo.
5. Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma?
6. Enyi milima, mruke kama kondoo waume? Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7. Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8. Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.

  Psalms (114/150)