Psalms (113/150)  

1. Haleluya. Enyi watumishi wa Bwana, sifuni, Lisifuni jina la Bwana.
2. Jina la Bwana lihimidiwe Tangu leo na hata milele.
3. Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa.
4. Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote, Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5. Ni nani aliye mfano wa Bwana, Mungu wetu aketiye juu;
6. Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani?
7. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8. Amketishe pamoja na wakuu, Pamoja na wakuu wa watu wake.
9. Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha.

  Psalms (113/150)