| ← Psalms (112/150) → |
| 1. | Haleluya. Heri mtu yule amchaye Bwana, Apendezwaye sana na maagizo yake. |
| 2. | Wazao wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. |
| 3. | Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yakaa milele. |
| 4. | Nuru huwazukia wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. |
| 5. | Heri atendaye fadhili na kukopesha; Atengenezaye mambo yake kwa haki. |
| 6. | Kwa maana hataondoshwa kamwe; Mwenye haki atakumbukwa milele. |
| 7. | Hataogopa habari mbaya; Moyo wake u imara ukimtumaini Bwana. |
| 8. | Moyo wake umethibitika hataogopa, Hata awaone watesi wake wameshindwa. |
| 9. | Amekirimu, na kuwapa maskini, Haki yake yakaa milele, Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu. |
| 10. | Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuyeyuka, Tamaa ya wasio haki itapotea. |
| ← Psalms (112/150) → |