| ← Psalms (110/150) → |
| 1. | Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako. |
| 2. | Bwana atainyosha toka Sayuni Fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako; |
| 3. | Watu wako wanajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako. |
| 4. | Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki. |
| 5. | Bwana yu mkono wako wa kuume; Ataseta wafalme, Siku ya ghadhabu yake. |
| 6. | Atahukumu kati ya mataifa, Ataijaza nchi mizoga; Ataseta kichwa katika nchi nyingi. |
| 7. | Atakunywa maji ya mto njiani; Kwa hiyo atakiinua kichwa chake. |
| ← Psalms (110/150) → |