← Psalms (108/150) → |
1. | Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Nitaimba, nitaimba zaburi, Naam, kwa utukufu wangu. |
2. | Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri. |
3. | Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu, Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa. |
4. | Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni, Na uaminifu wako hata mawinguni. |
5. | Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako. |
6. | Ili wapenzi wako waopolewe, Uokoe kwa mkono wako wa kuume, uniitikie. |
7. | Mungu amenena kwa utakatifu wake, Nami nitashangilia. Nitaigawanya Shekemu, Nitalipima bonde la Sukothi. |
8. | Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme, |
9. | Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita. |
10. | Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hata Edomu? |
11. | Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa? Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu? |
12. | Utuletee msaada juu ya mtesi, Maana wokovu wa binadamu haufai. |
13. | Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu. |
← Psalms (108/150) → |