| ← Psalms (105/150) → | 
| 1. | Haleluya. | 
| 2. | Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Zitafakarini ajabu zake zote. | 
| 3. | Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. | 
| 4. | Mtakeni Bwana na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote. | 
| 5. | Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya, Miujiza yake na hukumu za kinywa chake. | 
| 6. | Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake; Enyi wana wa Yakobo, wateule wake. | 
| 7. | Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake. | 
| 8. | Analikumbuka agano lake milele; Neno lile aliloviamuru vizazi elfu. | 
| 9. | Agano alilofanya na Ibrahimu, Na uapo wake kwa Isaka. | 
| 10. | Alilomthibitishia Yakobo liwe amri, Na Israeli liwe agano la milele. | 
| 11. | Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa. | 
| 12. | Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa, Naam, watu wachache na wageni ndani yake, | 
| 13. | Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. | 
| 14. | Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. | 
| 15. | Akisema, Msiwaguse masihi | 
| 16. | Akaiita njaa iijilie nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea. | 
| 17. | Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani. | 
| 18. | Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma. | 
| 19. | Hata wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya Bwana ilimjaribu. | 
| 20. | Mfalme alituma watu akamfungua, Mkuu wa watu akamwachia. | 
| 21. | Akamweka kuwa bwana wa nyumba yake, Na mwenye amri juu ya mali zake zote. | 
| 22. | Awafunge masheki wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima. | 
| 23. | Israeli naye akaingia Misri, Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu. | 
| 24. | Akawajalia watu wake wazae sana, Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao. | 
| 25. | Akawageuza moyo wawachukie watu wake, Wakawatendea hila watumishi wake. | 
| 26. | Akamtuma Musa, mtumishi wake, Na Haruni ambaye amemchagua. | 
| 27. | Akaweka mambo ya ishara zake kati yao, Na miujiza katika nchi ya Hamu. | 
| 28. | Alituma giza, kukafunga giza, Wala hawakuyaasi maneno yake. | 
| 29. | Aliyageuza maji yao yakawa damu, Akawafisha samaki wao. | 
| 30. | Nchi yao ilijaa vyura, Vyumbani mwa wafalme wao. | 
| 31. | Alisema, kukaja makundi ya mainzi, Na chawa mipakani mwao mwote. | 
| 32. | Badala ya mvua aliwapa mvua ya mawe, Na moto wa miali katika nchi yao. | 
| 33. | Akaipiga mizabibu yao na mitini yao, Akaivunja miti ya mipaka yao. | 
| 34. | Alisema, kukaja nzige, Na tunutu wasiohesabika; | 
| 35. | Wakaila miche yote ya nchi yao, Wakayala matunda ya ardhi yao. | 
| 36. | Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi, Malimbuko ya nguvu zao. | 
| 37. | Akawatoa hali wana fedha na dhahabu, Katika kabila zao asiwepo mwenye kukwaa. | 
| 38. | Misri ilifurahi walipoondoka, Maana kwa ajili yao hofu imewaangukia. | 
| 39. | Alitandaza wingu liwe funiko, Na moto utoe nuru usiku. | 
| 40. | Walipotaka akaleta kware, Akawashibisha chakula cha mbinguni. | 
| 41. | Akaufunua mwamba, kukabubujika maji, Yakapita pakavuni kama mto. | 
| 42. | Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Ibrahimu, mtumishi wake. | 
| 43. | Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha. | 
| 44. | Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu; | 
| 45. | Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake. Haleluya. | 
| ← Psalms (105/150) → |