Psalms (100/150)  

1. Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote;
2. Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba;
3. Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4. Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5. Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.

  Psalms (100/150)