← Proverbs (4/31) → |
1. | Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio mpate kujua ufahamu. |
2. | Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu. |
3. | Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu. |
4. | Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi. |
5. | Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu. |
6. | Usimwache, naye atakuhifadhi; Umpende, naye atakulinda. |
7. | Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu. |
8. | Umtukuze, naye atakukuza; Atakupatia heshima, ukimkumbatia. |
9. | Atakupa neema kuwa kilemba kichwani; Na kukukirimia taji ya uzuri. |
10. | Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi. |
11. | Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu. |
12. | Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa. |
13. | Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako. |
14. | Usiingie katika njia ya waovu, Wala usitembee katika njia ya wabaya. |
15. | Jiepushe nayo, usipite karibu nayo, Igeukie mbali, ukaende zako. |
16. | Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu. |
17. | Maana wao hula mkate wa uovu, Nao hunywa divai ya jeuri. |
18. | Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu. |
19. | Njia ya waovu ni kama giza; Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho. |
20. | Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu. |
21. | Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako. |
22. | Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote. |
23. | Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. |
24. | Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe. |
25. | Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa. |
26. | Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike; |
27. | Usigeuke kwa kuume wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni. |
← Proverbs (4/31) → |