← Numbers (26/36) → |
1. | Ikawa baada ya hilo pigo, Bwana akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia, |
2. | Fanya jumla ya mkutano wote wa wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani. |
3. | Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia, |
4. | Fanyeni jumla ya watu, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama Bwana alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri. |
5. | Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu; |
6. | na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi. |
7. | Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tatu elfu na mia saba na thelathini. |
8. | Na wana wa Palu; Eliabu. |
9. | Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na Bwana; |
10. | nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara. |
11. | Pamoja na hayo, hao wana wa Kora hawakufa. |
12. | Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini; |
13. | wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli. |
14. | Hizi ndizo jamaa za Wasimeoni, watu ishirini na mbili elfu na mia mbili. |
15. | Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni; |
16. | wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri; |
17. | wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli. |
18. | Hizi ndizo jamaa za wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, arobaini elfu na mia tano. |
19. | Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani. |
20. | Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera. |
21. | Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli. |
22. | Hizi ndizo jamaa za Yuda kama waliohesabiwa kwao, sabini na sita elfu na mia tano. |
23. | Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva; |
24. | wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni. |
25. | Hizi ndizo jamaa za Isakari kama waliohesabiwa kwao, sitini na nne elfu na mia tatu. |
26. | Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli. |
27. | Hizi ndizo jamaa za Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, sitini elfu na mia tano. |
28. | Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu. |
29. | Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi. |
30. | Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki; |
31. | na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu; |
32. | na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi. |
33. | Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na wana waume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa. |
34. | Hizi ndizo jamaa za Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni hamsini na mbili elfu na mia saba. |
35. | Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi. |
36. | Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani. |
37. | Hizi ndizo jamaa za wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, thelathini na mbili elfu na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao. |
38. | Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu; |
39. | wa Shufamu, jamaa ya Washufamu; wa Hufamu, jamaa ya Wahufamu. |
40. | Na wana wa Bela walikuwa Ardi na Naamani; wa Ardi, jamaa ya Waardi; wa Naamani, jamaa ya Wanaamani. |
41. | Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia sita. |
42. | Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao. |
43. | Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa sitini na nne elfu na mia nne. |
44. | Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia. |
45. | Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli. |
46. | Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera. |
47. | Hizi ndizo jamaa za wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, hamsini na tatu elfu na mia nne. |
48. | Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni; |
49. | wa Yeseri, jamaa ya Wayeseri, wa Shilemu jamaa ya Washilemu. |
50. | Hizi ndizo jamaa za Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini na tano elfu na mia nne. |
51. | Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, mia sita na moja elfu, na mia saba na thelathini (601,730). |
52. | Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, |
53. | Watu hawa watagawanyiwa nchi hiyo iwe urithi wao, vile vile kama hesabu ya majina yao ilivyo. |
54. | Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake. |
55. | Lakini nchi itagawanywa kwa kura; kwa majina ya kabila za baba zao, ndivyo watakavyopata urithi. |
56. | Kama kura itakavyokuwa, ndivyo urithi wao utakavyogawanywa kati yao, hao wengi na hao wachache. |
57. | Na hao waliohesabiwa katika Walawi kwa jamaa zao ni hawa; wa Gershoni, jamaa ya Wagershoni; na wa Kohathi, jamaa ya Wakohathi; na wa Merari, jamaa ya Wamerari. |
58. | Hizi ndizo jamaa za Lawi; jamaa ya Walibni, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya Wamala, na jamaa ya Wamushi jamaa ya Wakora. Na Kohathi alimzaa Amramu. |
59. | Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu umbu lao. |
60. | Tena kwake Haruni walizaliwa hawa, Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. |
61. | Tena Nadabu na Abihu wakafa, hapo waliposongeza moto wa kigeni mbele za Bwana. |
62. | Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa ishirini na tatu elfu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli. |
63. | Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko. |
64. | Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai. |
65. | Kwa kuwa Bwana alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni. |
← Numbers (26/36) → |