← Mark (7/16) → |
1. | Kisha Mafarisayo, na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele yake, |
2. | wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa. |
3. | Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao; |
4. | tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba. |
5. | Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi? |
6. | Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; |
7. | Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, |
8. | Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. |
9. | Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. |
10. | Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. |
11. | Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; |
12. | wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; |
13. | huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo. |
14. | Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu. |
15. | Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. |
16. | Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.] |
17. | Hata alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza habari za ule mfano. |
18. | Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; |
19. | kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. |
20. | Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. |
21. | Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, |
22. | wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. |
23. | Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. |
24. | Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika. |
25. | Ila mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu, alisikia habari zake, akaja akamwangukia miguuni pake. |
26. | Na yule mwanamke ni Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katika binti yake. |
27. | Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa. |
28. | Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto. |
29. | Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako. |
30. | Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka. |
31. | Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. |
32. | Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono. |
33. | Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, |
34. | akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. |
35. | Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. |
36. | Akawaonya wasimwambie mtu; lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari; |
37. | wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme. |
← Mark (7/16) → |