| ← Job (40/42) → |
| 1. | Bwana akafuliza kumjibu Ayubu, na kusema, |
| 2. | Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye. |
| 3. | Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema, |
| 4. | Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu. |
| 5. | Nimenena mara moja, nami sitajibu; Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi. |
| 6. | Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, |
| 7. | Jifunge viuno kama mwanamume, Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie. |
| 8. | Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha? Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki? |
| 9. | Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye? |
| 10. | Haya! Jivike sasa fahari na ukuu; Jipambe heshima na enzi. |
| 11. | Mwaga mafuriko ya hasira zako, Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili. |
| 12. | Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe, Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo. |
| 13. | Wafiche mavumbini pamoja, Wafunge nyuso zao mahali palipositirika. |
| 14. | Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako, Ya kuwa mkono wako wa kuume waweza kukuokoa. |
| 15. | Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe; Yeye hula nyasi kama vile ng'ombe, |
| 16. | Tazama basi, nguvu zake ni katika viuno vyake, Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake. |
| 17. | Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi; Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja. |
| 18. | Mifupa yake ni kama mirija ya shaba; Mbavu zake ni kama vipande vya chuma. |
| 19. | Yeye ni mkuu wa njia za Mungu; Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake. |
| 20. | Hakika milima humtolea chakula; Hapo wachezapo wanyama wote wa barani. |
| 21. | Hulala chini ya miti yenye vivuli, Mafichoni penye mianzi, na matopeni. |
| 22. | Hiyo miti yenye vivuli humfunika kwa vivuli vyao; Mierebi ya vijito humzunguka. |
| 23. | Tazama, mto ukifurika, yeye hatetemeki; Hujiona yu salama, ijapokuwa Yordani hufurika hata kinywani pake. |
| 24. | Je! Mtu ye yote atamnasa akiwa yu macho, Au, kumtoboa pua yake kwa mtego? |
| ← Job (40/42) → |