← Job (37/42) → |
1. | Moyo wangu hunitetema kwayo pia, Nao hutoka mahali pake. |
2. | Zisikizeni hizo kelele za sauti yake, Na uvumi utokao kinywani mwake. |
3. | Yeye huituma iende chini ya mbingu zote, Na radi yake hata miisho ya nchi. |
4. | Baadaye sauti hunguruma; Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake; Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo. |
5. | Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake; Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuelewa nayo. |
6. | Kwani huiambia theluji, Anguka juu ya nchi; Na vivyo manyonyota ya mvua, Na hayo maji ya mvua yake kubwa. |
7. | Huufunga mkono wa kila binadamu; Ili watu wote aliowaumba wajue. |
8. | Hapo wanyama huingia mafichoni, Na kukaa katika mapango yao. |
9. | Dhoruba hutoka katika vyumba vyake; Na baridi ghalani mwake. |
10. | Barafu huletwa kwa pumzi za Mungu; Na upana wa maji huganda. |
11. | Naam, huyatweka mawingu mazito mzigo wa maji; Hulitandika wingu la umeme wake; |
12. | Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake, Ili yafanye yote atakayoyaagiza Juu ya uso wa dunia hii ikaayo watu; |
13. | Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake, Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye. |
14. | Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu. |
15. | Je! Wajua wewe jinsi Mungu anavyoziagiza, Na kuumulikisha umeme wa wingu lake? |
16. | Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa? |
17. | Jinsi nguo zako zilivyo na moto, Hapo nchi ituliapo kwa sababu ya upepo wa kusini? |
18. | Je! Waweza kuzitandaza mbingu pamoja naye, Ambazo zina nguvu kama kioo cha kuyeyushwa? |
19. | Utufundishe ni maneno gani tutakayomwambia; Kwa maana hamwezi kuyatengeza kwa sababu ya giza. |
20. | Je! Aambiwe kwamba nataka kunena? Au mtu angetamani kumezwa? |
21. | Na sasa watu hawawezi kuutazama mwanga ung'aao mbinguni; Lakini upepo ukipita huzitakasa. |
22. | Kaskazini hutokea umemetufu wa dhahabu; Mungu huvikwa ukuu utishao. |
23. | yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea. |
24. | Kwa hiyo watu humwogopa; Yeye hawaangalii walio na hekima mioyoni. |
← Job (37/42) → |