| ← Job (35/42) → | 
| 1. | Tena Elihu akajibu na kusema, | 
| 2. | Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako, Au je! Wasema, Haki yangu ni zaidi kuliko ya Mungu, | 
| 3. | Maana wasema, Kutakuwa na faida gani kwako wewe? Tena, Nitapata faida gani, kuliko nikifanya dhambi? | 
| 4. | Mimi nitakujibu, Na hawa wenzio pamoja nawe. | 
| 5. | Ziangalie mbingu ukaone; Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe. | 
| 6. | Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Yakiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye? | 
| 7. | Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani? Au yeye hupokea nini mkononi mwako? | 
| 8. | Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe; Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu. | 
| 9. | Kwa sababu ya wingi wa jeuri wao hulia; Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu. | 
| 10. | Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu, Awapaye nyimbo wakati wa usiku; | 
| 11. | Atufundishaye zaidi ya hayawani wa nchi, Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege za angani? | 
| 12. | Hulia huko, lakini hapana ajibuye, Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu. | 
| 13. | Hakika Mungu hatasikia ubatili, Wala Mwenyezi hatauangalia. | 
| 14. | Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii, Hiyo daawa i mbele yake, nawe wamngojea! | 
| 15. | Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujilia katika hasira zake, Wala hauangalii sana unyeti; | 
| 16. | Ndiposa Ayubu hufunua kinywa chake kwa ubatili; Huongeza maneno pasipo maarifa. | 
| ← Job (35/42) → |