Job (25/42)  

1. Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2. Enzi na hofu zi pamoja naye; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.
3. Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?
4. Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?
5. Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake;
6. Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!

  Job (25/42)