| ← Job (24/42) → |
| 1. | Mbona nyakati zisiwekwe na Mwenyezi? Na hao wamjuao mbona hawazioni siku zake? |
| 2. | Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi kwa jeuri na kuyalisha. |
| 3. | Humfukuza punda wake asiye baba, Humtwaa rehani ng'ombe wake mwanamke mjane. |
| 4. | Humgeuza mhitaji aiache njia; Maskini wa nchi hujificha pamoja. |
| 5. | Tazama, kama punda-mwitu jangwani Wao hutoka kwenda kazini mwao, wakitafuta chakula kwa bidii; Jangwa huwapa chakula cha watoto wao. |
| 6. | Hukata nafaka zao mashambani; Na kuokota zabibu za waovu. |
| 7. | Hujilaza usiku kucha uchi pasipo nguo, Wala hawana cha kujifunika baridi. |
| 8. | Hutota kwa manyunyo ya milimani, Na kuambatana na jabali kwa kukosa sitara, |
| 9. | Wako wamwondoao matitini kwa nguvu huyo asiye na baba, Na kutwaa rehani kwa maskini; |
| 10. | Hata wazunguke uchi pasipo mavazi, Nao wakiwa na njaa huchukua miganda; |
| 11. | Hushindika mafuta ndani ya makuta ya watu hao; Wakanyaga mashinikizo, nao wana kiu. |
| 12. | Watu huugua toka mji ulio na watu wengi, Na roho yake aliyejeruhiwa hupiga ukelele; Wala Mungu hauangalii upumbavu. |
| 13. | Hawa ni katika hao waliouasi mwanga; Hawazijui njia zake, Wala hawakai katika mapito yake. |
| 14. | Mwuaji huamka asubuhi kukipambauka, huwaua maskini na wahitaji; Tena wakati wa usiku yu kama mwivi. |
| 15. | Tena jicho lake mzinifu hungojea wakati wa giza-giza, Akisema, Hapana jicho litakaloniona; Naye huuficha uso wake. |
| 16. | Wao hutoboa nyumba gizani; Hujifungia ndani wakati wa mchana; Hawaujui mwanga. |
| 17. | Kwani asubuhi kwao wote ni kama giza tupu; Kwani wao wavijua vitisho vya hiyo giza tupu. |
| 18. | Mwasema, Yeye ni mwepesi juu ya uso wa gharika; Sehemu yao inalaaniwa duniani; Hageuki kwenda njia ya mizabibuni. |
| 19. | Chaka na hari hukausha maji ya theluji; Kuzimu nako hao ambao wamefanya dhambi. |
| 20. | Tumbo lililomzaa litamsahau; buu litamla na kuona tamu; Hatakumbukwa tena; Na udhalimu utavunjwa kama mti. |
| 21. | Naam, yeye huwala walio tasa wasiozaa; Wala hamtendei mema mwanamke mjane. |
| 22. | Lakini Mungu huwadumisha wenye uwezo kwa nguvu zake; Huinuka, wasiokuwa na tumaini la kuishi. |
| 23. | Huwapa kuwa na salama, nao wapumzika kwayo; Na macho yake ya juu ya njia zao. |
| 24. | Wao wametukuzwa; lakini kitambo kidogo hutoweka; Naam, hushushwa, na kuondolewa njiani kama wengine wote, Nao hukatwa kama vile masuke ya ngano. |
| 25. | Na kama sivyo sasa, ni nani atakayenihukumu kuwa ni mwongo, Na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu? |
| ← Job (24/42) → |