| ← Job (17/42) → |
| 1. | Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma, Kaburi i tayari kunipokea. |
| 2. | Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka, Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao. |
| 3. | Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe; Kuna nani atakayeniwekea dhamana? |
| 4. | Kwani mioyo yao imeificha ufahamu; Kwa hiyo hutawakuza. |
| 5. | Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo, Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi. |
| 6. | Amenifanya niwe simo kwa watu; Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi. |
| 7. | Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli. |
| 8. | Walekevu watayastaajabia hayo, Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu. |
| 9. | Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu. |
| 10. | Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa; Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu. |
| 11. | Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika, Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu. |
| 12. | Wabadili usiku kuwa mchana; Wasema, Mwanga u karibu kwa sababu ya giza. |
| 13. | Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu; Nikitandika malazi yangu gizani; |
| 14. | Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu; Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na umbu langu; |
| 15. | Basi, tumaini langu li wapi? Na tumaini langu, ni nani atakayeliona? |
| 16. | Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu, Itakapokuwapo raha mavumbini. |
| ← Job (17/42) → |