| ← Job (13/42) → |
| 1. | Tazama, jicho langu limeyaona hayo yote, Sikio langu limeyasikia na kuelewa nayo. |
| 2. | Hayo myajuayo ninyi, na mimi pia nayajua; Mimi si duni kuliko ninyi. |
| 3. | Hakika ningenena naye huyo Mwenyezi, Nami nataka kuhojiana na Mungu. |
| 4. | Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo, Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa. |
| 5. | Laiti mngenyamaza kabisa! Hilo lingekuwa hekima kwenu. |
| 6. | Sikieni sasa basi hoja zangu, Mkayasikie mashindano ya midomo yangu. |
| 7. | Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu, Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake? |
| 8. | Je! Mtamwonyesha yeye upendeleo? Mtamtetea Mungu? |
| 9. | Je! Itafaa yeye kuwatafuta ninyi? Au, kama kumdanganya mtu, je! Mtamdanganya yeye? |
| 10. | Hakika atawakemea ninyi, Mkiwapendelea watu kwa siri. |
| 11. | Je! Huo ukuu wake hautawatia hofu, Na utisho wake hautawaangukia? |
| 12. | Matamko yenu ya hekima ni mithali ya majivu, Ngome zenu ni ngome za udongo. |
| 13. | Nyamazeni, niacheni, ili nipate kunena, Na hayo yatakayonijilia na yaje. |
| 14. | Nitaitwaa nyama ya mwili wangu katika meno yangu, Na kuutwaa uhai wangu mkononi mwangu! |
| 15. | Tazama, ataniua; sina tumaini; |
| 16. | Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu; Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake. |
| 17. | Sikieni sana maneno yangu, Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu. |
| 18. | Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu, Najua ya kuwa ni mwenye haki mimi. |
| 19. | Yuko nani atakayeshindana nami? Maana sasa nitanyamaa kimya na kutoa roho. |
| 20. | Lakini msinifanyie mambo mawili, hayo tu, Ndipo nami sitajificha usoni pako; |
| 21. | Uondoe mkono wako usinilemee; Na utisho wako usinitie hofu. |
| 22. | Basi uite wakati huo, nami nitaitika; Au, niache ninene mimi, nawe unijibu. |
| 23. | Maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi? Nijulishe kosa langu na dhambi yangu. |
| 24. | Mbona umeuficha uso wako, Na kunihesabu kuwa ni adui yako? |
| 25. | Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo? Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu? |
| 26. | Kwani umeandika maneno ya uchungu juu yangu, Na kunirithisha maovu ya ujana wangu; |
| 27. | Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyaaua mapito yangu yote; Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu; |
| 28. | Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa, Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo. |
| ← Job (13/42) → |