← Isaiah (18/66) → |
1. | Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa, Iliyoko mbali kupita mito ya Kushi; |
2. | Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji. |
3. | Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni. |
4. | Maana Bwana ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa jua kali, mfano wa wingu la umande katika hari ya mavuno. |
5. | Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata. |
6. | Wote pamoja wataachiwa ndege wakali wa milimani, na hayawani wa nchi; ndege wakali watakaa juu yao wakati wa jua, na hayawani wote wa nchi watakaa juu yao wakati wa baridi. |
7. | Wakati huo Bwana wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao; |
← Isaiah (18/66) → |