| ← Isaiah (12/66) → |
| 1. | Na katika siku hiyo utasema, Ee Bwana, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo. |
| 2. | Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. |
| 3. | Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. |
| 4. | Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litajeni jina lake kuwa limetukuka. |
| 5. | Mwimbieni Bwana; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote. |
| 6. | Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako. |
| ← Isaiah (12/66) → |