| ← Hosea (12/14) → |
| 1. | Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri. |
| 2. | Bwana naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa. |
| 3. | Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu; |
| 4. | Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko; |
| 5. | Naam, Bwana, Mungu wa majeshi; Bwana ndilo kumbukumbu lake. |
| 6. | Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima. |
| 7. | Ni mchuuzi, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu. |
| 8. | Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi. |
| 9. | Lakini mimi ni Bwana, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi. |
| 10. | Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano. |
| 11. | Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng'ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba. |
| 12. | Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu, Na Israeli alitumika apate mke; Ili apate mke alichunga kondoo. |
| 13. | Na kwa nabii Bwana alimtoa Israeli katika Misri, Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa. |
| 14. | Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake. |
| ← Hosea (12/14) → |