← Genesis (9/50) → |
1. | Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi. |
2. | Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu. |
3. | Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. |
4. | Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile. |
5. | Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu. |
6. | Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu. |
7. | Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake. |
8. | Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema, |
9. | Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu; |
10. | tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi. |
11. | Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi. |
12. | Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; |
13. | Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. |
14. | Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, |
15. | nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. |
16. | Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. |
17. | Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi. |
18. | Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani. |
19. | Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu. |
20. | Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; |
21. | akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. |
22. | Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. |
23. | Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. |
24. | Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. |
25. | Akasema, |
26. | Akasema, |
27. | Mungu akamnafisishe Yafethi. |
28. | Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini. |
29. | Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa. |
← Genesis (9/50) → |