| ← Genesis (5/50) → | 
| 1. | Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; | 
| 2. | mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. | 
| 3. | Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. | 
| 4. | Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. | 
| 5. | Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa. | 
| 6. | Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi. | 
| 7. | Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake. | 
| 8. | Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa. | 
| 9. | Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani. | 
| 10. | Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake. | 
| 11. | Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa. | 
| 12. | Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. | 
| 13. | Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake. | 
| 14. | Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa. | 
| 15. | Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. | 
| 16. | Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake. | 
| 17. | Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa. | 
| 18. | Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. | 
| 19. | Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. | 
| 20. | Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa. | 
| 21. | Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. | 
| 22. | Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. | 
| 23. | Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. | 
| 24. | Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. | 
| 25. | Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki. | 
| 26. | Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake. | 
| 27. | Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa. | 
| 28. | Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana. | 
| 29. | Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana. | 
| 30. | Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake. | 
| 31. | Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa. | 
| 32. | Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi. | 
| ← Genesis (5/50) → |