← Genesis (36/50) → |
1. | Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ndiye Edomu. |
2. | Esau alitwaa binti za Kanaani, kuwa wakeze; Ada, binti Eloni, Mhiti, na Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, Mhivi; |
3. | na Basemathi, binti Ishmaeli, nduguye Nebayothi. |
4. | Ada akamzalia Esau Elifazi; na Basemathi alizaa Reueli. |
5. | Oholibama alizaa Yeushi, na Yalamu, na Kora. Hao ndio wana wa Esau aliozaliwa katika nchi ya Kanaani. |
6. | Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng'ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye. |
7. | Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao. |
8. | Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu. |
9. | Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri. |
10. | Haya ndiyo majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reuli, mwana wa Basemathi, mkewe Esau. |
11. | Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi. |
12. | Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau. |
13. | Na hawa ni wana wa Reueli, Nahathi, na Zera, na Shama na Miza. Hao walikuwa wana wa Basemathi, mkewe Esau. |
14. | Na hawa ni wana wa Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, mkewe Esau; akamzalia Esau, Yeushi, na Yalamu, na Kora. |
15. | Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi, |
16. | jumbe Kora, jumbe Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio majumbe, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada. |
17. | Na hawa ni wana wa Reueli, mwanawe Esau; jumbe Nahathi, jumbe Zera, jumbe Shama, jumbe Miza. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Basemathi, mkewe Esau. |
18. | Na hawa ni wana wa Oholibama, mkewe Esau; jumbe Yeushi, jumbe Yalamu, jumbe Kora. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau. |
19. | Hao ni wana wa Esau, na hao ndio majumbe wao; naye Esau ndiye Edomu. |
20. | Hawa ni wana wa Seiri, Mhori, wenyeji wa nchi ile; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, |
21. | na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, wana wa Seiri, katika nchi ya Edomu. |
22. | Na wana wa Lotani, ni Hori, na Hemamu; na umbu lake Lotani ni Timna. |
23. | Na hawa ni wana wa Shobali, Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. |
24. | Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye. |
25. | Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana. |
26. | Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. |
27. | Na hawa ni wana wa Eseri, Bilhani, na Zaawani, na Akani. |
28. | Na hawa ni wana wa Dishani, Usi, na Arani. |
29. | Hawa ndio majumbe waliotoka katika Wahori; jumbe Lotani, jumbe Shobali, jumbe Sibeoni, jumbe Ana, |
30. | jumbe Dishoni, jumbe Eseri jumbe Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, kwa habari za majumbe yao, katika nchi ya Seiri. |
31. | Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli. |
32. | Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba. |
33. | Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake. |
34. | Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake. |
35. | Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi. |
36. | Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake. |
37. | Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake. |
38. | Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake. |
39. | Akafa Baal-hanani, mwana wa Akbori, akamiliki Hadadi badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. |
40. | Na hayo ndiyo majina ya majumbe waliotoka kwa Esau, kufuata jamaa zao, na mahali pao, kwa majina yao. Jumbe Timna, jumbe Alva, jumbe Yethethi, |
41. | jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni, |
42. | jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibsari, |
43. | jumbe Magdieli, jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu, kufuata makao yao, katika nchi ya mamlaka yao. Naye huyo ndiye Esau, baba ya Edomu. |
← Genesis (36/50) → |