← Genesis (10/50) → |
1. | Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. |
2. | Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. |
3. | Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. |
4. | Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. |
5. | Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao. |
6. | Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. |
7. | Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani. |
8. | Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. |
9. | Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana. |
10. | Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari. |
11. | Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala; |
12. | na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa. |
13. | Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, |
14. | na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori. |
15. | Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi, |
16. | na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi, |
17. | na Mhivi, na Mwarki, na Msini, |
18. | na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana. |
19. | Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha. |
20. | Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao. |
21. | Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana. |
22. | Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu. |
23. | Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. |
24. | Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi. |
25. | Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani. |
26. | Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera, |
27. | na Hadoramu, na Uzali, na Dikla, |
28. | na Obali, na Abimaeli, na Seba, |
29. | na Ofiri, na Havila, na Yobabi. Hao wote ndio wana wa Yoktani. |
30. | Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki. |
31. | Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao. |
32. | Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika. |
← Genesis (10/50) → |