← Ecclesiastes (10/12) → |
1. | Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima. |
2. | Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto. |
3. | Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu. |
4. | Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; |
5. | Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; |
6. | ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini. |
7. | Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa. |
8. | Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma. |
9. | Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo. |
10. | Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa. |
11. | Nyoka akiuma asijatumbuizwa, Basi hakuna faida ya mtumbuizi. |
12. | Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake. |
13. | Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari. |
14. | Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza? |
15. | Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja, Maana hajui hata njia ya kuuendea mji. |
16. | Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi! |
17. | Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi. |
18. | Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja. |
19. | Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote. |
20. | Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo lako; Wala usiwalaani wakwasi chumbani mwako; Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti, Na mwenye mabawa ataitoa habari. |
← Ecclesiastes (10/12) → |