Ecclesiastes (1/12) → |
1. | Maneno ya Mhubiri |
2. | Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. |
3. | Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua? |
4. | Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. |
5. | Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. |
6. | Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake. |
7. | Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena. |
8. | Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia. |
9. | Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. |
10. | Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi. |
11. | Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye. |
12. | Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. |
13. | Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. |
14. | Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo. |
15. | Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki. |
16. | Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa. |
17. | Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo. |
18. | Yaani, |
Ecclesiastes (1/12) → |