| ← Deuteronomy (33/34) → |
| 1. | Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake. |
| 2. | Akasema, |
| 3. | Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako. |
| 4. | Musa alituagiza torati, Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo. |
| 5. | Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja. |
| 6. | Reubeni na aishi, asife; Lakini watu wake na wawe wachache. |
| 7. | Na baraka ya Yuda ni hii; akasema, Isikize, Ee Bwana, sauti ya Yuda, Umlete ndani kwa watu wake; Alijitetea kwa mikono yake; Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake. |
| 8. | Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta naye kwenye maji ya Meriba. |
| 9. | Aliyemtaja baba yake na mama yake, Mimi sikumwona; Wala nduguze hakuwakubali; Wala hakuwajua watoto wake mwenyewe; Maana wameliangalia neno lako, Wamelishika agano lako. |
| 10. | Watamfundisha Yakobo hukumu zako, Na Israeli torati yako, Wataweka uvumba mbele zako, Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako. |
| 11. | Ee Bwana, ubariki mali zake, Utakabali kazi ya mikono yake; Uwapige viuno vyao waondokao juu yake, Na wenye kumchukia, wasiinuke tena. |
| 12. | Akamnena Benyamini, Mpenzi wa Bwana atakaa salama kwake; Yuamfunika mchana kutwa, Naye hukaa kati ya mabega yake. |
| 13. | Na Yusufu akamnena, Nchi yake na ibarikiwe na Bwana; Kwa vitu vya thamani vya mbinguni, kwa huo umande, Na kwa kilindi kilalacho chini, |
| 14. | Na kwa vitu vilivyo bora vya matunda ya jua, Na kwa vitu vilivyo bora vya maongeo ya miezi, |
| 15. | Na kwa vitu viteule vya milima ya kale, Na kwa vitu vilivyo bora vya vilima vya milele, |
| 16. | Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake, Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kijiti; Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze. |
| 17. | Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase. |
| 18. | Na Zabuloni akamnena, Furahi Zabuloni, katika kutoka kwako; |
| 19. | Watayaita mataifa waje mlimani; Wakasongeze huko sadaka za haki; Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari, Na akiba zilizofichamana za mchangani. |
| 20. | Na Gadi akamnena, Na abarikiwe amwongezaye Gadi; Yeye hukaa kama simba mke, Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa. |
| 21. | Akajichagulia sehemu ya kwanza, Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria; Akaja pamoja na wakuu wa watu, Akaitekeleza haki ya Bwana, Na hukumu zake kwa Israeli. |
| 22. | Na Dani akamnena, Dani ni mwana-simba, Arukaye kutoka Bashani. |
| 23. | Na Naftali akamnena, Ee Naftali, uliyeshiba fadhili, Uliyejawa na baraka ya Bwana; Umiliki magharibi na kusini. |
| 24. | Na Asheri akamnena, Na abarikiwe Asheri kwa watoto; Na akubaliwe katika nduguze, Na achovye mguu wake katika mafuta. |
| 25. | Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako. |
| 26. | Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni, Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie. Na juu ya mawingu katika utukufu wake. |
| 27. | Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza. |
| 28. | Na Israeli anakaa salama, Chemchemi ya Yakobo peke yake, Katika nchi ya ngano na divai; Naam, mbingu zake zadondoza umande. |
| 29. | U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu. |
| ← Deuteronomy (33/34) → |