← Colossians (3/4) → |
1. | Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. |
2. | Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. |
3. | Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. |
4. | Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. |
5. | Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; |
6. | kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu. |
7. | Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo. |
8. | Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. |
9. | Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; |
10. | mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. |
11. | Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote. |
12. | Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, |
13. | mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. |
14. | Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. |
15. | Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. |
16. | Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. |
17. | Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. |
18. | Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. |
19. | Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. |
20. | Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana. |
21. | Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa. |
22. | Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana. |
23. | Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, |
24. | mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo. |
25. | Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo. |
← Colossians (3/4) → |