← 2Timothy (4/4) |
1. | Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; |
2. | lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. |
3. | Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; |
4. | nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. |
5. | Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. |
6. | Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. |
7. | Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; |
8. | baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. |
9. | Jitahidi kuja kwangu upesi. |
10. | Maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia. |
11. | Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi. |
12. | Lakini Tikiko nalimpeleka Efeso. |
13. | Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi. |
14. | Iskanda, mfua shaba, alionyesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake. |
15. | Nawe ujihadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu. |
16. | Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. |
17. | Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. |
18. | Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina. |
19. | Nisalimie Priska na Akila, na wale wa nyumbani mwa Onesiforo. |
20. | Erasto alikaa Korintho. Trofimo nalimwacha huko Mileto, hawezi. |
21. | Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi. Eubulo akusalimu, na Pude, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia. |
22. | Bwana na awe pamoja na roho yako. Neema na iwe pamoja nanyi. |
← 2Timothy (4/4) |