← 2Timothy (3/4) → |
1. | Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. |
2. | Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, |
3. | wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, |
4. | wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; |
5. | wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. |
6. | Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; |
7. | wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli. |
8. | Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani. |
9. | Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri. |
10. | Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu, |
11. | na upendo, na saburi; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote. |
12. | Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. |
13. | lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. |
14. | Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; |
15. | na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. |
16. | Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; |
17. | ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. |
← 2Timothy (3/4) → |