← 2Samuel (23/24) → |
1. | Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa Yese, anena, Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu, Yeye, masihi |
2. | Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu. |
3. | Mungu wa Israeli alisema, Mwamba wa Israeli aliniambia, Atawalaye wanadamu kwa haki, Akitawala katika kicho cha Mungu, |
4. | Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo, Asubuhi isiyo na mawingu. |
5. | Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za Bwana? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; Ina taratibu katika yote, ni thabiti, Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote. |
6. | Lakini hatawachipuza watu wa ubatili; Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa, Ambayo haivuniki kwa mkono, |
7. | Mtu atakayeigusa hiyo, Na awe na chuma na mpini wa mkuki, Nao watateketezwa papo hapo kwa moto. |
8. | Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu |
9. | Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao; |
10. | huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu. |
11. | Na baada yake kulikuwa na Shama, mwana wa Agee, Mharari; nao Wafilisti walikuwa wamekusanyika huko Lehi, palipokuwapo konde lililojaa midengu; nao watu wakawakimbia Wafilisti; |
12. | ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye Bwana akafanya wokovu mkuu. |
13. | Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai. |
14. | Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu. |
15. | Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango! |
16. | Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana. |
17. | Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu. |
18. | Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu. |
19. | Je! Huyo hakuwa na heshima maalumu miongoni mwa wale watatu? Kwa hiyo akawekwa kuwa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. |
20. | Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu, |
21. | huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe. |
22. | Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu. |
23. | Alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake. |
24. | Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu; |
25. | na Shama, Mharodi, na Elika, Mharodi; |
26. | na Helesi, Mpeloni, na Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi; |
27. | na Abiezeri, Mwanathothi, na Sibekai, Mhushathi; |
28. | na Salmoni, Mwahohi, na Maharai, Mnetofathi; |
29. | na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini; |
30. | na Benaya, Mpirathoni, na Hurai, wa vijito vya Gaashi; |
31. | na Abieli, Mwarbathi, na Azmawethi, Mbarhumi; |
32. | na Eliaba, Mshaalboni, na wana wa Yasheni; na Yonathani, |
33. | mwana wa Shama, Mharari, na Ahiamu, mwana wa Shalali, Mharari; |
34. | na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni; |
35. | na Hezro, Mkarmeli, na Paarai, Mwarbi; |
36. | na Igali, mwana wa Nathani, wa Soba, na Bani, Mgadi; |
37. | na Seleki, Mwamoni, na Naharai, Mbeerothi, ambao ni wachukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya; |
38. | na Ira, Mwithri, na Garebu, Mwithri; |
39. | na Uria, Mhiti; jumla yao ilikuwa watu thelathini na saba. |
← 2Samuel (23/24) → |