← 2Samuel (22/24) → |
1. | Basi Daudi akamwambia Bwana maneno ya wimbo huu, siku ile Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake zote, na mkononi mwa Sauli; |
2. | akasema, Bwana ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu, naam, wangu; |
3. | Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri. |
4. | Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu. |
5. | Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. |
6. | Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili. |
7. | Katika shida yangu nalimwita Bwana, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu; |
8. | Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasuka-suka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu. |
9. | Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala; Makaa yakawashwa nao. |
10. | Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake. |
11. | Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo. |
12. | Akafanya giza hema zake za kumzunguka, Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni. |
13. | Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Makaa ya moto yakawashwa. |
14. | Bwana alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye juu akaitoa sauti yake. |
15. | Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatapanya. |
16. | Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake Bwana, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake. |
17. | Alipeleka kutoka juu, akanishika; Akanitoa katika maji mengi; |
18. | Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia; Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi. |
19. | Walinikabili siku ya msiba wangu; Lakini Bwana alikuwa tegemeo langu. |
20. | Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami. |
21. | Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa. |
22. | Maana nimezishika njia za Bwana, Wala sikumwasi Mungu wangu. |
23. | Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu; Na kwa habari za amri zake, sikuziacha. |
24. | Nami nalikuwa mkamilifu kwake, Nikajilinda na uovu wangu. |
25. | Basi Bwana amenilipa sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake. |
26. | Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu; |
27. | Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi. |
28. | Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa; Ila macho yako ni juu ya wenye kiburi, uwadhili. |
29. | Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee Bwana; Na Bwana ataniangazia giza langu. |
30. | Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi; Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta. |
31. | Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya Bwana imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia. |
32. | Maana ni nani aliye Mungu, ila Bwana? Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu? |
33. | Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake. |
34. | Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. |
35. | Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba. |
36. | Nawe umenipa ngao ya wokovu wako; Na unyenyekevu wako umenikuza. |
37. | Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Wala miguu yangu haikuteleza. |
38. | Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza; Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa. |
39. | Nami nimewakomesha na kuwapiga-piga wasiweze kusimama; Naam, wameanguka chini ya miguu yangu. |
40. | Maana umenifunga mshipi wa nguvu kwa vita; Umenitiishia chini yangu walioniondokea. |
41. | Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo, Ili niwakatilie mbali wanaonichukia. |
42. | Walitazama, lakini hakuna wa kuokoa; Walimwita Bwana, lakini hakuwajibu. |
43. | Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi, Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya. |
44. | Nawe umeniokoa na mashindano ya watu wangu; Umenihifadhi niwe kichwa cha mataifa; Watu nisiowajua watanitumikia. |
45. | Wageni watanijia wakinyenyekea; Kwa kusikia tu habari zangu, Mara watanitii. |
46. | Wageni nao watatepetea, Watatoka katika ngome zao wakitetemeka. |
47. | Bwana ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa mwamba wa wokovu wangu; |
48. | Naam, Mungu anipatiaye kisasi, Na kuwatweza watu chini yangu, |
49. | Na kunileta nje nitoke kwa adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia; Waniponya na mtu wa jeuri. |
50. | Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako. |
51. | Ampa mfalme wake wokovu mkuu; Amfanyia fadhili masihi |
← 2Samuel (22/24) → |