← 2Corinthians (6/13) → |
1. | Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. |
2. | (Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; |
3. | Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe; |
4. | bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida; |
5. | katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; |
6. | katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki; |
7. | katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; |
8. | kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli; |
9. | kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa; |
10. | kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote. |
11. | Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa. |
12. | Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu. |
13. | Basi, ili mlipe kadiri ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), nanyi pia mkunjuliwe mioyo. |
14. | Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? |
15. | Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? |
16. | Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. |
17. | Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. |
18. | Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, |
← 2Corinthians (6/13) → |